Rapa 50 Cent Anahitaji Kusahau Kabisa Kundi Lake La Zamani G-UNIT


Nguli wa HipHop 50cent amefuta uwezekano wa kuwepo kwa Filamu maalumu itayoongelea Maisha ya Kundi Lake la Zamani G-UNIT , baada ya kusema kuwa anahitaji kulisahau kundi hilo kwasasa .

50 Cent ameongea hayo alipokua katika Mahojiano na Dj Whoo Kid , baada ya kuulizwa kuhusu mipango ya Filamu (Flick) ya G-UNIT .

“ Sijali kuhusu G-Unit, natamani kusahau Kuhusu G-Unit kwasasa “ - alisema 50 .

Hata hivyo baada ya Jibu hilo Dj Whoo Kid Alishangazwa na kumuambia 50 Cent kuwa atawakatili Mashabiki , kwasababu wanatamani kuona Filamu hiyo .

Inaelezwa kuwa 50cent na baadhi ya Wasanii wenzake waliokua wanaunda Kundi la G-Unit (Young Bucks, Loyd Banks na Tony Yayo) Hawapo katika maelewano mazuri kwasasa , na haioneshi kama wanaweza kupatana hivi Karibuni !


EmoticonEmoticon