R.Kelly Aripotiwa Kukanyagwa Kichwani Huku Akiwa karibu Achomwe Na Kitu Kichwani

Wiki iliyopita taarifa kutoka gereza la Metropolitan mjini Chicago zilisema mwimbaji mkongwe R. Kelly ambaye anashikiliwa hapo wakati akisubiri kesi yake ya unyanyasaji wa kingono, alivamiwa na kushambuliwa vibaya na mfungwa mwenzake akiwa gerezani.

Sasa kwa mujibu wa taarifa mpya kutoka mtandao wa Page Six, imeripotiwa kwamba mfungwa huyo alikutwa akimkanyaga kichwani Kellz na baada ya hapo kutaka kumchoma na kalamu lakini walifanikiwa kumzuia.

Kwa hali hiyo, mwanasheria wa Kellz, Steven Greenberg aliiomba mahakama kumuachia mteja wake kwa dhamana.


EmoticonEmoticon