Soma Makosa Vijana Wengi Hufanya Wanapokua Wamepata Pesa

Huenda vijana wengi wakafanya makosa wanapoendelea kukua ama wamepata kazi ya kuwapa riziki yao ya kila siku si wote lakini baadhi yao hufanya makosa na kisha wajuta baadaye.

Wazungu hawakukosea waliposema msemo wao ‘I wish i knew comes later’ vijana wengi ugundua kuwa muda umeenda na wameharibu wakati wao mwingi kwa mambo yasiostahili.

Haya hapa makosa ambayo vijana wengi hufanya wanapokuwa, na kama utapata kuna makosa ambayo unayafanya na kutajwa haya basi rekebisha mwenendo wako kabla ya muda hujayoyoma na kisha kuja kujuta.

1.Mapenzi
Wengi husema ya kwamba mapenzi ni kipofu, lakini vijana wengi hawafahamu kuwa wanaharibu wakati wao wanapopenda ilhali hawaoni uhusiano wao unawapeleka kiwango kingine.
Kwa kweli wazungu hawakukosea waliposema kuwa ‘love is blind’ lakini wakasahau kusema kila kijana anapaswa kuwa makini na maisha yake.

2.Kutumia pesa kwa mambo yasio faa
Baadhi ya vijana wakipata mshahara wao hupenda kununua mitindo ya nguo ya hivi majuzi ili wasionekane kama wako nyuma, pia wanaponunua nguo mpya wanaunua zenye bei ya juu
Pia wengi hupenda kuhudhuria sherehe tofauti huku wakibwagia vileo na kuwanunulia marafiki zao bila ya kujali ya kesho.

3.Kujaribu kupendeza kila mtu
Kwa maana wanataka kupendwa na kila jinsia na mtu kwa hivyo lazima wafanye lolote au chochote ili kupendeza kila mtu huku wakisahau ya kwamba muda unakwenda kwa kasi na kushtukia wamepitwa na wakati.

4.Kuwalaumu wazazi kwa misiba na kutofanikiwa kwao
Kama wewe ni kajana amka mapema nenda ukatie bidii kazini huku ukijua na kufahamu kuwa unajenga maisha yako na wala si ya wazazi wako.
Utapata vijana wengi wasipofanikiwa wanawalaumu wazazi wao kwa hayo yote na kusahau kuwa wanapaswa kutia bidii ili kutoka katika hali duni ya maisha.

5.Kutoka weka akiba
Huwa wanasema ukiwa na pesa tumia ikuzoee, na kisha kusahau kama wana maisha ya kesho na kutoweka akiba ya maisha yao.


EmoticonEmoticon