Kampuni ya
Marekani ya Oracle imeikataa Kampuni ya Microsoft na kuingia makubaliano ya
ushirikiano wa kibiashara (Business Partner) na kampuni ya China inayomiliki
Mtandao wa TikTok, hii ni baada ya Rais Donald Trump kutaka Tiktok iuziwe
Wamarekani la sivyo ataifunga isifanye kazi nchini humo.
Hata hivyo, haijafahamika
iwapo ushirikiano huo wa TikTok na Oracle kama mshirika wa teknolojia
unamaanisha kwamba Oracle itakuwa na hisa kubwa zaidi katika umiliki wa
shughuli hiyo ya kimtandao.
Kampuni ya Microsoft ya
Marekani ilikuwa inachukuliwa kama kampuni ya teknolojia ya Marekani yenye
uwezo wa kununua shughuli za TikTok nchini Marekani kutoka katika kampuni-mama
yake, ya ByteDance, na yenye uwezo mkubwa zaidi wa kushughulikia masuala ya
usalama wa taifa, jambo lililosababisha uamuzi huo wa Trump.
EmoticonEmoticon