Trump Atembelea Mji Ambao Mmarekani Mweusi Alipigwa Risasi Na Kuunga Mkono Polisi

Rais wa Marekani Donald trump amezuru Kenosha, Wisconsin, kuunga mkono utekelezaji wa sheria baada ya kitendo cha polisi kumpiga risasi mwanaume mweusi kusababisha maandamano. 

Rais alitembelea maeneo yaliyoharibiwa na waandamanaji, ikiwemo duka la samani lililotiwa moto wakati wa maandamano.

"Haya si matendo ya maandamano ya amani, bali ni ugaidi wa ndani," aliwaambia viongozi wa biashara katika mkutano wa pamoja uliofanyika kwenye mazoezi ya viungo ya shule ya sekondari.

Rais alionesha huruma kidogo kwa walioumia wakati wa makabiliano na polisi, akisema anahisi vibaya kwa yeyote yule anayepitia hayo. Lakini alisema haamini kwamba kuna mfumo wa kibaguzi katika utekelezaji wa sheria.Bwana Trump alisema alituma jeshi la ulinzi wa Taifa huko Kenosha, ingawa lilipelekwa na gavana wa Wisconsin na kuungwa mkono na maafisa 200 wa serikali kulingana na agizo la rais.

Alisema utawala wake utatoa karibu dola milioni 4 kusaidia biashara za mji wa Kenosha ambazo zimeharibiwa na vurugu na uporoji huku dola milioni 1 ikitengewa mji huo kwa utekelezaji wa sheria.

Waandamanaji hao wameshutumu waandamanaji kutoka nje ya mji walioteka nyara maandamano yao. mwishoni mwa juma lililopita, polisi ilisema washukiwa 105 kati a 175 waliokamatwa wakati wa aandamano walikuwa wanatoka nje ya mji.


EmoticonEmoticon