Ufaransa Mwenyeji Wa Mkutano Wa Mataifa Ya Mediterania

Kundi  la  EuroMed7 ni kundi  ambalo si rasmi la  mataifa  saba  ya Umoja  wa  Ulaya  yanayopakana  na  bahari  ya  Mediterania, baadhi  ya  nyakati  yakijulikana  kama " klabu ya Med",  ambayo yalifanya  mara  ya  kwanza  mkutano  wao mwaka  2016 na ambayo  hayaijumishi  Uturuki. 

Lakini mkutano huo  katika  kisiwa  cha  Ufaransa  cha  Corsica kitawaleta  pamoja  viongozi wa  Ufaransa, Italia, malta, Ureno na Uhispania pamoja  na  wanachama wa Umoja  wa  Ulaya  wa mataifa  ya  mashariki  mwa  bahari ya Mediterania Ugiriki  na Cyprus.

Ufaransa imeiunga  mkono  kwa  nguvu  Ugiriki  na  Cyprus  katika mkwamo  unaoongezeka  pamoja na  Uturuki kuhusiana  na  maliasili ya  gesi  na  mafuta  pamoja  na  ushawishi  wa  jeshi  la  majini katika  eneo  la  mashariki  mwa  Mediterania ambao umezusha  hofu za mzozo.

Mkutano  huo  utafanyika  leo mchana  katika  mji  wa  pwani  wa kitalii  nje  kidogo  ya  mji  mkuu  wa  jimbo  la  Corsica, Ajaccio.

Lengo  la  mazungumzo  hayo  ni  "kupiga  hatua  katika  kupata muafaka  juu  ya  uhusiano  wa  Umoja  wa  Ulaya  na  Uturuki  ikiwa pamoja  na  yote  kabla ya  mkutano  wa  Septemba  24-25 wa Umoja  wa  Ulaya,"  afisa  wa  ofisi  ya  rais  wa  Ufaransa amesema.


EmoticonEmoticon