Ujerumani Yatoboa Siri Kubwa, Kiongozi Wa Upinzani Urusi Alitiliwa Sumu Ya Novichok, Kansela Merkel Atoa Neno

Viongozi kutoka kote ulimwenguni wamelaani tukio la kupewa sumu kiongozi wa upinzani Urusi Alexei Navalny katika jaribio la kutaka kumuuwa. 

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema anatarajia Urusi kueleza msimamo wake

Kansela Merkel amesema kulikuwa na "habari za kutisha” zilizoonesha "bila shaka yoyote" kuwa tukio la kupewa sumu Alexei Navalny lilikuwa "jaribio la mauaji kwa kutumia sumu inayoathiri mishipa ya fahamu” baada ya vipimo vya nchini Ujerumani kuonyesha kuwa sumu ya Novichok ilitumika dhidi ya kiongozi huyo wa upinzani. 

Merkel amesema Navalny ni "muhanga wa uhalifu ulionuia kumnyamazisha,” akiongeza kuwa ukubwa wa suala hilo ni muhimu kwake "kuchukua msimamo wa wazi”. 

Hatima ya Alexei Navalny imevutia hisia za ulimwengu wote. Ulimwengu utasubiri majibu. Tutawafahamisha washirika wetu wa EU na NATO kuhusu matokeo haya ya uchunguzi. 

Tutashauriana na kuamua hatua mwafaka ya pamoja tutakayochukua kwa kutegemea na kuhusika kwa Urusi. Uhalifu dhidi ya Alexei Navalny ni kinyume na maadili na haki za msingi tunazozilinda.

Merkel amesema kisa hicho kinaibua maswali muhimu sana ambayo ni serikali ya Urusi pekee inayoweza kujibu. Vipimo hivyo vilifanywa katika maabara maalum ya jeshi la Ujerumani. Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani Heiko Maas mapema jana alimuita balozi wa Urusi Berlin kujadili hali hiyo.


EmoticonEmoticon