Umoja Wa Ulaya, China Kufanya Mkutano Wa Kilele Leo

Ulaya yafanya mazungumzo na China, ikitafuta kujiweka kati ya Marekani na China, kulinda maslahi yake ya kibiashara, huku pia ikisimamia maadili ya demokrasia na ya haki za binadamu

Mkutano wa kilele kati ya Umoja wa Ulaya na China unafanyika leo kwa njia ya video, ukifupishwa na kuwa wa siku moja kutoka tatu ilizopangiwa awali. 

Katika mkutano hao viongozi wa Ulaya wanakabiliwa na mtihani wa kuweka wizani kati ya maslahi ya biashara kusimamia maadili ya haki za binadamu. 

Kabla ya mlipuko wa virusi vya corona, mkutano huu wa kilele ulitarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 13 hadi 15 Septemba mjini Leipzig mashariki mwa Ujerumani, ambako, kwa mara ya kwanza rais Xi Jinping wa China angezungumza ana kwa ana na viongozi wote wa nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya, na ungeonyesha nguvu za kansela wa Ujerumani Angela Merkel, katika wadhifa wake kama rais wa Umoja wa Ulaya wakati huu. 

Lakini sasa mkutano huo unafanyika kwa njia ya video, tena kwa siku moja tu. Kansela Merkel ataungana na rais wa baraza la Ulaya Charles Michel na rais wa Halmashauri ya Ulaya Ursula von der Leyen, na upande mwingine utakuwa na rais Xi Jinping akiwaongoza maafisa wa China.


EmoticonEmoticon