Wafungwa Congo Wanakufa Kwaajili Ya Njaa

Ukosefu wa chakula kwenye Magereza mbalimbali Congo umetajwa kusababisha vifo vya Wafungwa na Mahabusu ambapo Watu wawili wamefariki wiki hii katika Gereza la Bunia na kufanya idadi ya waliofia Gerezani hapo kufikia Watu 17 tangu April mwaka huu hadi leo.

"Watu kutoka Kanisani wanapoleta chakula ndio tunafurahia lakini hali ni mbaya, tunaishi kimasikini, tunalala pabaya, hatuli, hatuzingatii ulinzi wa afya zetu, nguo tunazigeuza sahani, tunashindia vijiko viwili vya uji siku nzima, ukiletwa ubwabwa wa Kanisa kwetu ni sikukuu" - MAHABUSU

Kwa mujibu wa Umoja wa Afrika, Watu 201 walifia Gerezani Congo mwaka 2017 na mwaka 2018 walifariki 223, huku chanzo kikubwa kikitajwa kuwa ni ukosefu wa chakula na dawa.


EmoticonEmoticon