Wanyama Pori Wanaangamia Kwa Kasi, Imeonya Ripoti

Idadi ya wanyama pori imepungua kwa zaidi ya thuluthi mbili katika kipindi kisichopungua miaka 50 , kulingana na ripoti muhimu ya kundi la uhifadhi wa wanyama pori WWF.

Ripoti hiyo inasema kwamba kushuka kwa idadi hiyo hakuoneshi ishara za kupungua.
Na imeonya kwamba asili inaharibiwa na wanadamu kiwango ambacho a hakijawahi kuonekana awali.
Wanyama pori wanapungua kwasababu ya uchomaji wa miti, kuvua samaki kupita kiasi, na kufanya uharibifu katika maeneo ambayo wanyama pori wanaishi kulingana na Tanya Steele, afisa mkuu mtendaji katika WWF.
''Tunaharibu dunia yetu mahali tunapoita nyumbani - tukihatarisha afya yetu , usalama na kuishi duniani''.
''Sasa asili inatutumia ujumbe wa kwamba muda unayoyoma''.
''Upungufu huo ni ushahidi tosha wa uharibifu unaofanywa na wanadamu katika asili ya duniani'' , alisema Dkt. Andrew Terry , mkurugenzi wa uhifadhi katika mbuga ya wanyama ya London ambayo ilitoa takwimu hizo.


EmoticonEmoticon