Waziri Mkuu Wa Mpya wa Japan Baada Ya Shinzo Abe

Bunge la Japan limemchagua Yoshihide Suga kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo, kufuatia hatua ya Shinzo Abe kujiuzulu.

Baada ya kushinda uongozi wa chama tawala mapema wiki hii, kura ya Jumatano imeidhinisha rasmi wadhifa wa mkuu huyo zamani wa mawaziri.
Waziri mkuu huyo mpya ambaye ni mshirika wa karibu wa bwana Abe, anatarajiwa kuendeleza sera ya mtangulizi wake.
Shinzo Abe alitangazi kujiuzulu kwake mwezi uliopita kutokana na sababu za afya.
Mapema Jumatano, Bw. Abe alifanya mkutano wake wa mwisho wa mawaziri na kuwaambia wanahabari kwamba anajivunia utawala wake wa karibu miaka minane.
Bwana Suga alishinda kirahisi katika uchaguzi wa waziri mkuu katika bunge la Diet, ambalo ni la chini nchini Japan, baada ya kupata 314 kati ya kura zote 462 zilizopigwa
Ikizingatiwa kwamba muungano unaoongozwa na chama chake cha kihafidhina, Liberal Democratic Party (LDP) kina wabunge wengi, ushindi wake ulitarajiwa na wengi.
Yeye pamoja na mawaziri wake wapya baadaye wataidhinishwa rasmi katika hafla itakayoandaliwa katika Imperial Palace.


EmoticonEmoticon