Waziri Wa Elimu Kenya Aagiza Vyuo Vikuu Na Taasisi Za Kadri Za Elimu Kufunguliwa Okotoba 5

Waziri wa elimu nchini Kenya George Magoha ameagiza baadhi ya vyuo vikuu na taasisi za kadri kufunguliwa Jumatatu wiki ijayo kama moja wapo ya taratibu za serikali kufunguliwa kwa taasisi za elimu nchini humo.

Waziri alisema kwamba wanafunzi wote waliotarajiwa kufanya mitihani ya mwisho mwaka huu katika vyuo vya walimu na vyuo vya anuai watarejea vyuoni Jumatatu wiki ijayo.Alisema kwamba bodi za vyuo anuai na vile vya walimu zitatangaza kurejea vyuoni kwa wanafunzi wa miaka mingine ya chini huku kipau mbele kikipewa wanafunzi wanaofanya kozi tekelezi. 

Wanafunzi wa miaka ya mwisho katika vyuo vikuu na taasisi na zingine pia wanatarajiwa kurejea siku ya Jumatatu.Waziri aliongeza kwamba seneti za kila chuo kikuu zitatangza siku ya kurejea kwa wanafunzi wengine.

Anasema kanuni zote za afya zinafaa kuzingatiwa kabla ya kufunguliwa kwa chuo chochote.Waziri alisema kwamba taasisi zote za elimu zitalazimika kuhakikisha kwamba kanuni zote za wizra ya afya kudhibiti maambukizi ya Covid-19 zinazingatiwa ikiwemo kuchukuwa vipimo vya joto vya wanafunzi.

Taasisi zote ambazo zilikuwa zikitumika kama vituo vya karantini zitanyunyizwa dawa katika zoezi litakalo simamiwa na maafisa wa wizara wa wizara ya afya kabla ya kufunguliwa.

Credit:Radiojambo


EmoticonEmoticon