WHO Na Afrika CDC Yazindua Mtandao Wa Maabara Ya Covid-19

Shirika la Afya Duniani (WHO) ana Kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa Afrika (CDC) zimezindua mtandao mpya wa maabara ambayo itaimarisha mpangilio wa uchunguzi wa virusi vya corona barabi Afrika.

Mpango huo unachunguza uwezekano wa kuzaana kwa virusi vya corona ili kujiandaa vyema kutoa huduma katika sekata ya afya ya umma.

Wataalamu kutoka WHO na kituo cha CDC Afrika wanaamini hatua hiyo itasaidia nchi kuelewa tofauti kati ya chembe chembe ya virusi vya SARS na vile vya Cov-2, ili kuimarisha uwezo wa nchi kujitayarisha kwa matibabu au uwezekano wa kupata chanjo.

Maabara 12 maalum zitajumuishwa kwenye mtandao huo barani Afrika.

Hatua hiyo inakuja baada ya CDC Afrika kusema kuwa ripoti za awali zilikuwa zinaonesha kuwa viwango vya maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 vinashuka katika hali ambayo imepunguza idadi ya watu wanaoambukizwa virusi na wale wanaofariki kutokana na virusi hivyo ikilinganishwa na maeneo mengine dunani.

WHO hata hivyo imeonya hatua ya kusherehekea mapema matokeo hayo kwasababu baadhi ya nchi za Afrika haziwafanyii vipimo raia wao ikilinganishw ana maeneo mengine duniani.


EmoticonEmoticon