CORONA : Shirika La Afya Duniani (WHO) Yaripoti Ongezeko La Maambukizi Mapya Ndani Ya Saa 24

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa limerekodi ongezeko maambukizi mapya ya virusi vya corona kwa muda wa siku moja na kupata vifo zaidi ya 5,500, na kufanya dunia kuwa na jumla ya vifo 917,417 vilivyotokana na mlipuko huo.

Ongezeko kubwa la maambukizi limeripotiwa kutoka India, Marekani na Brazil.
Duniani kote kuna zaidi ya wagonjwa milioni 28 waliothibitika kuwa na virusi vya corona na nusu ya idadi hiyo ni kutoka Marekani.
Rekodi ya siku moja ya maambukizi mapya ilikuwa ya Septemba 6, wakati WHO iliporipoti maambukizi mapya 306,857.


EmoticonEmoticon