Afrika Kusini Yafungua Mipaka Kwa Nchi Za Afrika

 

Afrika Kusini imefungua mipaka yake kwa wasafiri kutoka nchi za Afrika, lakini imedumisha vikwazo dhidi ya nchi ambazo zina viwango vya juu vya maambukizi ya corona ikiwa ni pamoja na Uingereza, Marekani na Urusi.

Nchi hiyo ilifunga mipaka yakemwezi Machi mwaka huu katika juhudi za kuzuia kuenea kwa virusi.

Kuanzia leo Alhamisi Afrika Kusini itafungua baadhi ya mipaka yake ya ardhini viwanja vyake vikuu vya ndege Cape Town, Durban na Johannesburg.

Waziri wa mambo ya nje, Naledi Pandor, amesema wasafiri wote watakaowasili watalazimika kuonesha cheti cha kuthibitisha wamefanyiwa vipimo vya Covid-19 kutoka nchi zao na pia watafanyiwa ukaguzi watakapofika nchini humo.

Nchi ambazo viwango vya maambukizi ya virusi na vifo viko juu kuliko Afrika Kusini hawataruhusiwa kuzuru nchi hiyo kwa shughuli za utalii.


EmoticonEmoticon