Ahukimiwa Kwenda Jela Miaka 6 Kwa Kutembea Na Wanawake 19

 

Mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la Danny C Perry II (41) kutoka nchini Marekani, amehukumiwa kifungo cha miaka 6 jela kwa kosa la kutembea na wanawake 19 bila ya kutumia kinga na kutowaambia wanawake hao kama ana virusi vya ugonjwa wa Ukimwi. 

Taarifa za polisi zinasema Danny C Perry II  aliweza kutembea na wanawake wasiopungua 19 kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita, ambapo mpenzi wake wa kwanza alisema mwanaume huyo amekuwa akiishi na virusi hivyo tangu mwaka 2003.

Katika uamuzi wa Jaji wa makosa ya Jinai ya Mahakama kwenye Kaunti ya Davidson, Kate Boston amesema mtuhumiwa hakutumia kinga kwa makusudi wakati anajua ana virusi vya Ukimwi.

Alikusudia kumuambukiza mtu na virusi vya ukimwi, alijua anaugua maradhi hayo, na alifahamu vyema kwamba angewakinga wenzake dhidi ya kupata ugonjwa huo. Lakini alichagua kuhatarisha maisha ya wenzake” amesema Jaji Kate Boston

Aidha kwa upande wa mmoja wa wapenzi wake wa zamani aitwaye Marvelyn Brown ametoa ushuhuda kuhusu tukio hilo na amefurahi kuona amefungwa kifungo hicho kwani aliambukizwa ugonjwa huo na mwanaume huyo.


EmoticonEmoticon