Aliyekuwa Mbunge wa Burundi Anashikiliwa na Mamlaka Kwa Jaribio La Kupindua Serikali

 

Aliyekuwa mbunge wa Burundi Fabien Banciryanino anazuiliwa katika kituo cha polisi kwa kile ambacho inasemekana ni jaribio la kupindua serikali, kwa mujibu wa familia.

Bwana Banciryanino alikamatwa Ijumaa baada ya mkutano na wanahabari aliokuwa ameuitisha siku hiyo kufutwa, mwanafamilia wa karibu amezungumza na BBC.

Alichukuliwa na polisi kutoka nyumbani kwake katika mji mkuu wa Bunjumbura, mwanafamilia huyo aliongeza.

Polisi bado haijasema lolote kuhusu tamko hilo.

Mwanaume huyo aliyekuwa mbunge alikuwa mkosoaji wa aliyekuwa rais Pierre Nkurunziza, aliyefariki dunia Juni mwaka huu. Aidha, alipinga sheria yenye kumwezesha Bwana Nkurunziza kunufaika baada ya kustaafu kwake ikiwemo kuwa "kiongozi mkuu wa uzalendo".

Mkutano wake na wanahabari Ijumaa ulikuwa ni kuhusu kuzungumzia madai ya kituo kimoja cha eneo cha YouTube kwamba alimtukana rais, Evariste Ndayishimiye, kulingana na mwana familia.


EmoticonEmoticon