Mtu wa kwanza kutibiwa virusi vya ukimwi HIV - Timothy Ray Brown amefariki kutokana na saratani.
Bwana Brown ambaye pia alijulikana kama mgonjwa wa Berlin
alipandikizwa uboho kutoka kwa mtu ambaye alikuwa na kinga dhidi ya HIV 2017.
Hii
ilimaanisha kwamba alikuwa ahitaji tena dawa za kukabiliana na virusi vya
ukimwi hivyobasi alisalia bila maambukizi yoyote ya virusi hivyo
vinavyosababisha ukimwi kwa maisha yake yote.
Shirika
la kimataifa kuhusu wagonjwa wa ukimwi duniani limesema kwamba bwana Brown
aliupatia ulimwengu matumaini kwamba dawa ya kutibu ukimwi inaweza kupatikana.
Bwana Brown
mwenye umri wa miaka 54, ambaye alizaliwa nchini Marekani , alipatikana na
virusi vya HIV alipokuwa akiishi Berlin 1995.
Na
baadaye mwaka 2007 alipata saratani ya damu kwa jina Myeloid Leukemia. Tiba
yake ilianza kuharibu uboho wake ambao ulikuwa ukizalisha seli hizo za saratani
kabla ya kufanyia upandikizaji.
Uboho huo ulitoka kwa mfadhili ambaye alikuwa na mabadiliko nadra katika sehemu ya DNA iitwayo jeni ya CCR5.
EmoticonEmoticon