Armenia, Azerbaijan Zaendeleza Mapigano Licha Mpango Wa Usitishwaji Uhasama

 

Mapigano ya kugombania jimbo linalotaka kujitenga la Nagorno-Karabakh yameendelea, bila kuzuiwa na mpango wa kuweka chini silaha uliosimamiwa na Marekani, wakati Armenia na Azerbaijan zikitupiana lawama kwa kusambaratika kwa makubaliano hayo. 

Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Azerbaijan iliishutumu Armenia kwa kulishambulia kwa makombora eneo la Barda, na kuwauwa raia wanne, akiwemo msichana mwenye umri wa miaka miwili na kuwajeruhi wengine 13. 

Wizara ya Ulinzi ya Armenia ilikanusha tuhuma hizo ikisema ni uwongo mtupu na uchochezi mbaya. Katika hotuba kwa taifa jana, Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinian aliapa kuwa wanajeshi wa Nagorno-Karabakh watafanya mashambulizi ya kujibu ambayo yatasababisha uharibifu kwa adui.


EmoticonEmoticon