Baba Mwenye Nyumba Auwa Wapangaji Wake Wawili Kisa Kelele

 

Baba Mmoja Mwenye Nyumba huko Michigan Nchini Marekani, anashikiliwa na Polisi baada ya Kuwaua Wapangaji wake (Wapenzi) Wawili kwasababu aliyoitaja kuwa huwa wanampigia Kelele Usiku na kumfanya ashindwe kulala .

Muuaji huyo aliyefahamika kwa Jina la Chad Reed , Miaka 53 , alijasilimisha mwenyewe Polisi na kutoa maelezo kuwa hakuwaua kwa kukusudia bali alikua anajilinda Kutokana na Wapangaji hao kumtolea kisu baada ya kwenda kuwaomba wapunguze kelele ili aweze kulala .

Taarifa za Polisi zinasema kuwa Chad aliwaua Wapangaji wake hao kwa Bunduki , na sababu alizotoa ni kuwa wawili hao wamekuwa wakimnyima usingizi Kutokana na kelele nyingi wanazopiga Usiku ikiwemo kufungulia Muziki kwa Sauti ya Juu .


EmoticonEmoticon