Benki Kuu Yaidhinisha Dola Bilioni 12 Kugharamia Chanjo Kwa Nchi Masikini

 

Benki kuu ya Dunia imeidhinisha dola bilioni 12 kutoa msaada wa kifedha kwa nchi zinazoendelea kununua na kusambaza chanjo, kupima na kutoa matibabu, kwa lengo la kusaidia utoaji wa chanjo kwa hadi watu bilioni 1. 

Fedha hizo ni sehemu ya mpango mpana wa kundi la Benki kuu ya Dunia wa hadi dola bilioni 160 kusaidia nchi zinazoendelea kupambana na janga la COVID-19, benki hiyo imesema katika taarifa jana jioni. 

Benki kuu ya dunia imesema mpango wa kuchukua hatua za dharura dhidi ya COVID-19 tayari umezifikia nchi 111. Taarifa hiyo imesema raia katika nchi hizo zinazoendelea pia wanahitaji maji safi na chanjo sahihi ya COVID-19. 

Benki kuu imesema kuwa Shirika la fedha la kimataifa, ambalo ni tawi la sekta ya binafsi la benki hiyo kuu linawekeza katika utengenezaji wa chanjo kupitia mpango wenye thamani ya dola bilioni 4 wa jukwaa la afya duniani.


EmoticonEmoticon