Beyonce Awalilia Wa Nigeria Kwa Matukio Yanayoendelea

 

Beyonce ni miongoni mwa watu maarufu ambao wamelivalia njuga suala la mauaji ya wananchi nchini Nigeria yanayofanywa na Askari wa Kikosi maalum cha SARS.

Kupitia tovuti yake, Beyonce amesema ameumizwa sana na kinachoendelea nchini humo, akiahidi kushirikiana na washirika wake kupeleka misaada ya dharura ya huduma ya Afya, Chakula na Malazi.

"Nimevunjika moyo kuona uonevu wa kipuuzi unaoendelea nchini Nigeria. Ni lazima SARS ikomeshwe. Tumekuwa tukilifanyia kazi suala la mahusiano na taasisi za vijana kusaidia wote wanaoandamana kwa ajili ya mabadiliko. Tunashirikiana na washirika wetu kutoa huduma za dharura za Afya, Chakula na Malazi."


EmoticonEmoticon