Biden Amshutumu Trump Kwa Kushindwa Kushutumu Wazungu Wanaojiona Wao Ni Bora

 

Mgombea wa urais wa chama cha Democratic Joe Biden jana alimshutumu hasimu wake kutoka chama cha Republican Donald Trump kwa kushindwa kushutumu makundi ya wazungu wanaohisi wao ni jamii bora duniani wakati wa mdahalo wao wa kwanza uliogubikwa na mtafaruku. 

Biden alisema katika ukurasa wa Twitter kwamba hakuna njia nyingine ya kueleza, rais wa Marekani alikataa kujitenga na makundi hayo katika mjadala uliofanyika usiku wa jana. 

Baada ya kujibu kuwa ndio, Trump alilayaumu makundi ya mrengo wa kushoto kwa ghasia hizo za kisiasa, akipingana na taarifa za polisi. 

Kwa mujibu wa gazeti la New York Times wanachama wa makundi hayo wamesifu maneno ya Trump kama idhinisho la mbinu zao za kutumia nguvu katika mitandao ya kijamii ya binafsi, ambapo mtu mmoja alisema tayari wamepata wafuasi wapya. 

Jason Mille mshauri mwandamizi wa kampeni ya Trump, ameliambia gazeti hilo kwamba rais alikuwa na maana kwamba makundi hayo yaache tabia hiyo. 

Mtoto wa Trump Donald Trump Jr, amekiambia kituo cha televisheni cha CBS kuwa baba yake huenda alikosea kusema.


EmoticonEmoticon