Mwanasiasa na mwanamuziki wa Uganda,
Robert Kyagulanyi, al maarufu Bobi Wine, ameiambia BBC kuwa nyaraka
zinazohitajikakwa ajili ya uteuzi wake wa kugombea urais zimepotea katika ofisi
yake baada ya uvamizi wa ofisi hiyo wa vikosi vya usalama siku ya Jumatano
mchana.
Moja ya
masharti ya wagombea ni kuwasilisha sahihi za wafuasi wao 100 waliojisajili
kupiga kura kutoka katika walau theluthi mbili ya wilaya za Uganda.Bobi Wine
anasema timu yake ilikuwa tayari imekusanya sahihi milioni sita lakini hizi
sasa zimepotea.
“Serikali ya
Museveni inajaribu kunizuwia kuteuliwa kama mgombea wa urais. Kuanzia kuhoji
nyaraka zangu, kuhoji umri wangu- na sasa wanafanya kila juhudi kukwamisha
uteuzi wangu na ninaamini kuwa ndio maana walichukua saini .”
"Hatutakata
tamaa, tumekwisha ripoti mara mojakwa matawi yetukuhakikisha wanaanza kukusanya
saini mara mojana tunatumaini kufikia Ijumaa tutakuwa na saini zinazohitajika
,” alisema.
Mbunge huyo
alikuwa akizungumza na BBC baada ya kutoroka kutoka katika ofisi yake wakati
makumi kadhaa ya askari na polisi walipowasili kufanya msako.
Pia alisema
milioni 23 Waganda milioni ($6,200 ) zilichukuliwa. Anasema pesa hizi
zilichangishwa kusaidia kulipia garama za uchaguzi kwa ajili ya wanachama
wanaotaka kugombea ubunge.
Polisi
hawakujibu wito wa BBC wa kuzungumzia madai yaBobi Wine. Awali walikana kuwa
uvamizi wa ulichocjewa kisiasa.
Tume ya
uchaguzi iliwapatia wagombea siku ya Ijumaa kuwa muda wa mwisho wa kuwasilisha
fomu zao za uteuzi..
Msemaji wa tume anasema hawezi kuzungumzia juu ya madai ya Bobi Wine ya kutoweka kwa nyaraka lakini anasema muda wa mwisho unaweza uongezwa kwa mgombea iwapo wataifahamisha tume rasmi.
EmoticonEmoticon