Bomu La Vita Ya Pili Ya Dunia Lalipuka Kabla Ya Kuteguliwa

 

Bomu kubwa ambalo halikulipuka katika vita ya pili ya dunia lililobainika nchini Poland limelipuka wakati wa shughuli ya kulitegua, msemaji wa jeshi la wanamaji nchini humo ameeleza.

Uwezekano wa bomu hilo lililokuwa chini ya bahari kulipuka ulikuwa ukitarajiwa na wapiga mbizi wote waliohusika kwenye tukio hilo hawakujeruhiwa.

Karibu wakazi 750 waliondolewa karibu na mji wa bandari wa Swinoujscie.

Bomu hilo liitwalo Tallboy au ''tetemeko la ardhi'' lilidondoshwa wakati wa vita ya pili ya dunia na kuizamisha meli ya Ujerumani Lützow.

Swinoujscie ilikuwa sehemu ya Ujerumani na kuiita Swinemünde wakati wa ulipuaji.

Mtikisiko wakati wa kulitegua bomu hilo ulisikika katika sehemu za mji na video zinaonesha mlipuko mkubwa na maji mengi yakiruka angani.

Bomu hilo lilikuwa na urefu wa mita 6 na uzito wa tani 5.4, karibu nusu ya bomu hilo liliundwa na vilipuzi.

Lilikuwa limetua kwenye kina cha mita 12 na sehemu ya pua ya bomu hilo ilikua ikichungulia nje.


EmoticonEmoticon