Chris Brown Achukizwa Na Mashabiki Wanafiki, Awachana Live

Star wa R&B na Pop Duniani Chris Brown ametumia Ukurasa wake wa Instagram kuwachana wale watu/mashabiki ambao wanapenda kuwavaa Wasanii wanapoonesha Mali zao au Vitu vyao binafsi .

Kupitia ujumbe huo Chris amesema kuwa , ukiona mtu anachukia maisha ya Mtu binafsi basi huyo mtu ndio atakuwa ana matatizo .

Chris amesema ataendelea Kujiachia na Kuonyesha Maisha yake vile atakavyo , bila kujali mtu au Shabiki atasema nini !

"Mimi sio nyie na nyie hamuwezi kuwa mimi . Mnajindanganya kusema kuwa wote sisi ni sawa , hapana hatupo sawa . Nyamazeni na Msikilize Mziki " - amesema Chris katika "Povu" lake hilo kwa Mashabiki .


EmoticonEmoticon