Virusi
vinavyosababisha ugonjwa wa Covid 19 vinaweza kubaki kwenye vitu kama fedha za
karatasi, vioo vya simu na kwenye chuma kisichoshika kutu kwa siku 28, watafiti
wameeleza.
Matokeo
hayo ya shirika la kisayansi la taifa nchini Australia yanasema kuwa virusi vya
SARS-Cov-2 vinaweza kuishi kwa muda mrefu zaidi kuliko ilivyofikiriwa.
Hatahivyo,
jaribio hilo lilifanyika katika mazingira ya giza kwani mwanga wa UV tayari
ulishaonesha kuua virusi.
Baadhi
ya wataalamu wameonesha mashaka kuhusu tishio la maambukizi kupitia vitu hivyo
katika maisha ya kawaida.
Virusi
vya corona huambukiza watu wanapokohoa , kupiga chafya au kuzungumza.
Lakini pia kuna ushahidi kuwa virusi vinaweza kusambazwa kwa chembechembe zilizo kwenye hewa.
Pia inawezekana kuwa mtu anaweza kupata maambukizi kwa kugusa vitu au maeneo yenye virusi kama chuma au plastiki kwa mujibu wa vituo vya kudhibiti magonjwa vya nchini Marekani.
EmoticonEmoticon