Nyota wa timu ya Taifa ya Ureno
Cristiano Ronaldo amekutwa na maambukizi ya virusi vya Corona na ataukosa
mchezo wa Ligi ya Mataifa ya Ulaya dhidi ya Sweden kesho Jumatano.
Shirikisho la Soka
nchini Ureno (PFF) limetoa taarifa kwamba kwa sasa nyota huyo wa Klabu ya
Juventus anaendelea vizuri na hana dalili pia ametengwa peke yake. Wachezaji
wengine wamepata majibu hasi baada ya kupimwa leo Jumanne.
Jana Jumatatu CR7
ali-post picha/selfie hapa instagram akiwa na wachezaji wenzake wa timu ya
taifa ya Ureno wakiwa wanapata chakula cha pamoja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon