Daktari Wa Trump Athibitisha Maendelo Ya Raisi Huyo Akiwa Kwenye Matibabu Ya Covid-19

Rais wa Marekani Donald Trump "anaendelea vizuri" baada ya kuwa hospitali kwa usiku mmoja akiwa anaendelea kupata matibabu ya virusi vya corona.

Daktari wake binafsi Sean Conley amesema kwamba hapokei matibabu ya oksijeni na pia ndani ya kipindi cha saa 24, homa imeonesha kuisha.

Daktari Conley aliashiria matumaini makubwa sana kwa afya ya rais lakini akaongeza kwamba hawezi kusema ni lini ataruhusiwa kutoka hospitali.

Rais 74, ambaye ni mwanaume na aliye kwenye kundi la wenye uzito kupita kiasi, yuko miongoni mwa walio kwenye hatari ya juu ya kupata ugonjwa wa Covid-19.

Hadi kufikia sasa amekuwa akipata matibabu ya sindani na tiba ya kuzuia virusi ya remdesivir.

Mke wa rais Melania Trump, ambaye pia amethibitishwa kuapata maambukizi ya Covid-19, pia nae "anaendelea vizuri", amesema Daktari Conley. 


EmoticonEmoticon