Davido Adai Kwamba Wizkid Na Burnaboy Waungana Kumpindua

 

Mkali wa Muziki tokea nchini Nigeria 🇳🇬 Davido , amewashukia Mastaa Wenzake Wizkid na Burna Boy kwa kusema kuwa wanaungana ili kutaka kushinda nae Lakini hawatoweza kufanikiwa kwa hilo .

Akizungumza na kituo kimoja cha Tv nchini Nigeria, Davido amesema alijitahidi sana kuepuka Bifu baina yake na Burna Boy Pamoja na Wizkid , ila wawili hao wameendelea kumchukia bila sababu ya msingi .

“Unajua Burna Boy alikasirishwa na mimi kupost picha nikiwa na Wizkid Instagram. Mtu wake wa Karibu kabisa aliniambia kuwa 
Burbaboy hakupendezwa na Picha ile . Na sasa ivi yeye Pamoja na Wizkid wameungana ili kushindana na mimi Lakini nawambia hawatafanikiwa kwa hilo “ - alisema Davido katika mahojiano hayo .

Mpaka hivi sasa si W
izkid wala Burnaboy aliyeweza kujibu Mashambulizi ya kauli hii , ambayo kimsingi imeibua Bifu upya kati ya Marshall hawa watatu wa Muziki nchini Nigeria.


EmoticonEmoticon