Davido, Wizkid Waongoza Maandamano Nchini Nigeria

 

Nyota wa muziki nchini Nigeria, Davido na Wizkid kwa nyakati tofauti wameongoza sehemu ya maandamano ya vijana nchini humo kushinikiza kufutwa kwa Kikosi Maalumu cha Polisi cha Kupambana na Uhalifu (SARS), kutokana na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu hasa dhidi ya vijana katika utendaji wake.


Baada ya mfululizo wa maandamano ya barabarani na kauli za wasanii pia watu mashuhuri mitandaoni wakiwemo pia wasanii wa Marekani kama Diddy, Jeshi la polisi nchini Nigeria leo limetangaza kukisambaratisha Kikosi hicho na kukomesha kuendelea kwa shughuli zao. 


EmoticonEmoticon