Rais Donald
Trump wa Marekani, Jumamosi alipiga kura ya mapema kwenye kituo kimoja katika
jimbo la Florida, katika wikendi ambayo yeye na mpinzani wake, Makamu wa Rais
wa zamani Joe Biden, waliendelea kuhudhuria na kuhurubia mikutano katika miji
mbalimbali nchini, kunadi sera zao, kwelekea kwa uchaguzi wa tarehe tatu mwezi
ujao.
Trump, ambaye mwaka jana alibadilisha makazi yake rasmi
kutoka new York hadi Florida, alipiga kura mwendo wa asubuhi katika mji wa West
Palm Beach.
Alipoulizwa na waandishi wa Habari ni nani aliyempigia kura,
Trump alisema: "Nimempigia kura jamaa mmoja anayeitwa Trump," na
kuongeza kwamba "ni heshima kwangu kuweza kupiga kura.”
Biden naye amekita kambi katika jimbo lenye ushindani mkubwa
la Pennsylvania ambako amehutubia wafuasi wake na kumshutumu rais Trump kwa jinsi
alivyolishughulikia suala la janga la Corona.
Trump
anaelekea mjini Lumberton N Carolina, kwa mkutano wa kampeni, na baadaye kwenye
majimbo ya Ohio na Wisconsin.
Utafiti wa maoni unaonyesha kwamba bado kuna ushindani mkubwa kwenye baadhi ya majimbo, licha ya kwamba tayari zaidi ya Wamerakani milioni 50 walikuwa wamepiga kura za mapema kufikia Jumamosi asubuhi.
EmoticonEmoticon