Ethiopia Wakasirishwa Na Kauli Ya Trump Kulipua Bwawa La Nile

 

Waziri mkuu wa Ethiopia amesema nchi yake "haitakubali vitisho vya aina yoyote" baada ya Rais Donald Trump kusema kuwa Misri inaweza kuharibu bwawa lenye utata la Nile.

Bwawa hilo kubwa linakabiliwa na mzozo unaohusisha nchi za Ethiopia, Misri na Sudan. Bw. Trump alisema Misri haiwezi kuishi bila bwawa hilo na huenda "ikalipua" ujenzi huo.

Ethiopia inaohisi kuwa Marekani inapendelea Misri katika mzozo huo. Marekani ilitangaza mnamo mwezi Septemba kwamba itaipunguzia msaada Ethiopia baada ya nchi hiyo kuanza kujaza maji hifadhi iliyopo nyuma ya bwawa hilo mwezi Julai.


EmoticonEmoticon