Kutokana na mabadiliko ya mtindo wa
maisha, watu wengi hawapati muda wa kutosha wa kupumzika. Mara nyingi mtu
anapozidiwa hupunguza zaidi muda wa kupumzika ili akamilishe majukumu yake. Ikiwa unataka kuboresha utendaji
wako wa kazi pamoja na afya yako, fahamu faida 10 za kupumzika.
1. Huongeza uwezo wa kumbukumbu
Ubongo
wa mwanadamu unahitaji kupumzika ili uweze kujijenga na kufanya kazi vyema.
Ikiwa mtu hatapata muda wa kutosha wa kupumzika, uwezo wake wa kutunza
kumbukumbu utapungua.
2. Huondoa hatari ya kupata
kiharusi
Kiharusi
ni ugonjwa unaosababishwa na kupasuka kwa mishipa midogo ya damu kwenye ubongo;
hili husababisha damu kuvuja ndani ya ubongo.
3. Hulinda afya ya moyo
Kupumzika
kuna manufaa makubwa kwenye afya ya moyo wako. Ni wazi kuwa kasi ya usukumaji
wa damu wakati wa kufanya shughuli mbalimbali ni tofauti na wakati unapokuwa
umepumzika.
4. Hutoa muda wa mwili kujijenga
Miili
yetu inahitaji kujijenga kila mara hasa baada ya shughuli nyingi. Kwa njia ya
kupumzika utaweza kuupa mwili wako nafasi nzuri ya kujijenga na kurejeshha tena
nguvu iliyotumika wakati wa shughuli mbalimbali.
5. Huongeza hamasa ya utendaji
Nani
anapenda kufanya kazi akiwa amechoka? Naamini hakuna. Kupata muda wa kutosha wa
kupumzika kutakuwezesha kujisikia vizuri na kuwa tayari kutekeleza majukumu
yaliyoko mbele yako.
6. Huimarisha misuli
Tunapopumzika
misuli yetu inajijenga na kurudisha ute wake uliopotea wakati wa shughuli
mbalimbali. Hivyo ni muhimu kuhakikisha kila baada ya kazi tunapata muda wa
kutosha wa kupumzika ili tuboreshe afya za miili yetu.
7. Huimarisha kinga mwili
Kinga
mwili ni muhimu sana kwani hutuwezesha kukabiliana na magonjwa. Kwa njia ya
kupata muda wa kutosha wa kupumzika tunatoa nafasi kwa mfumo mzima wa kinga
mwili kujijenga na kujiimarisha.
8. Huondoa msongo wa mawazo
Chanzo
kimojawapo cha msongo wa mawazo ni uchovu, na chanzo kimojawapo cha maradhi
mbalimbali ni msongo wa mawazo.
9. Hutuwezesha kula vizuri
Ni
ukweli usiopingika kuwa tukiwa tumechoka hatuwezi kula vizuri. Hivyo kupata
muda mzuri na wakutosha wa kupumzika kutakuwezesha kula chakula vyema.
10. Huepusha ajali za barabarani
Je ulishasikia ajali zilizosababishwa na madereva wanaosinzia? Uchoovu na kukosa muda wa kupumzika (hasa kulala) humfanya mtu akose utulivu na uwezo wa kumudu chombo anachoedesha.
EmoticonEmoticon