Muigizaji Robert Pattinson amerejea
kwenye utayarishaji wa filamu ya The Batman mara baada ya
kusimama kwa muda kutokana na kugundulika kuwa na virusi vya COVID-19.
Pattinson ambaye
anacheza kama muhusika mkuu wa filamu hiyo amerejea kwenye eneo la utayarishaji
ikiwa ni wiki mbili tangu waongozaji watangaze kuendelea kwa shughuli hiyo ya
utayarishaji.
Pattinson amenaswa akiwa mjini Liverpool eneo la St. George Hall Filming kwenye
scene inayotajwa kuwa ya msiba akiwa amevalia suti nyeusi. The Batman inatajwa
kuachiwa March 4, 2022 mara baada ya kusogezwa mbele mara mbili kufuatia athari
za ugonjwa wa Corona.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon