Ghasia Zaibuka Nigeria Baada Ya Polisi Kuwafyatulia Risasi Waandamanaji

 

Majengo yamechomwa moto na kumeripotiwa kwa milio ya risasi katika miji mikubwa ya Nigeria wakati wa maandamano.

Shirika la kimataifa la Amnesty limesema watu wapatao 12 waliuawa na polisi na wanajeshi siku ya Jumannne.

Jeshi la Nigeria limekanusha ripoti hiyo na kudai kuwa ya uongo,waliandika katika kurasa ya Twitter.

Mamlaka iliweka amri ya kutotoka nje lakini baadhi walipuuzia agizo hilo. Waandamanaji dhidi ya polisi wamekuwa barabarani kwa kipindi cha wiki mbili sasa.

Waandamanaji wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kuhamasisha kampeni yao dhidi ya kikosi maalum cha polisi kinachojulikana kama Sars.

Rais Muhammadu Buhari alikisitisha kikosi hicho Oktoba 11. Lakini waandamanaji wameendelea na maandamano wakitaka mabadiliko zaidi katika vikosi vya usalama, pamoja na kubadilisha utendaji wao wa kazi.

Watu walioshuhudia milio ya risasi wameiambia BBC kuwa waliwaona jinsi polisi walivyokuwa wanamimina risasi Jumanne jioni.

Jumatano, baadhi ya majengo yalichomwa moto mjini Lagos na polisi waliweka zuio barabarani.

Kituo cha Televisheni Nigeria chenye uhusiano na chama tawala kilichomwa moto.

Polisi kutoka maeneo mbalimbnali walipiga risasi hewani ili kuwatawanyisha waandamanaji, mwandishi wa BBC Nduka Orjinmo anaripoti kutoka mji mkuu wa Abuja. Aliripoti pia kuna nyumba zilivamiwa na kuibiwa kwa viongozi kadhaa wa kijadi.


EmoticonEmoticon