Gwaride Kubwa La Kijeshi La Kuonyesh Silaha Korea Kaskazini Katika Historia Yake

 

Korea kaskazini inajiandaa kwa kile kinachotarajiwa kuwa gwaride kubwa la kijeshi katika historia yake .

Maelfu ya wanajeshi wamefanya mazoezi kwa miezi kadhaa ili kuhakikisha kuwa shughuli hiyo inafana mbele ya rais Kim jong-un.

Hafla hiyo hutumika kama onesho la uwezo wa kijeshi huku raia watiifu wakiendelea kumuheshimu kiongozi wao huku makosa yakiwa hayawezi kukubalika.

Taifa hilo halijaonyesha makombora yake ya masafa marefu katika magwaride yake tangu rais Donald Trump na Kim Jong-un walipofanya mkutano wao wa kwanza mnamo 2018.

Lakini gwaride hizi pia zinaweza kuwa njia ya sehemu ya uchokozi . Nafasi ya kuonyesha makombora na silaha mpya licha ya taifa hilo kuwa chini ya vikwazo vikali vya kiuchumi.

Mazungumzo kati ya pande hizo mbili yalivunjika huko Hanoi mnamo Februari iliyopita bila makubaliano na Korea Kaskazini imeendelea kufanyia majaribio makombora kadhaa ya masafa mafupi.

Hafla hii, inayofanyika tarehe 10 Oktoba, ili kuadhimisha miaka 75 ya kuanzishwa kwa Chama cha Wafanyakazi inajiri wiki chache kabla ya uchaguzi wa rais wa Marekani.


EmoticonEmoticon