Habari Tano Kubwa Za Michezo Jumanne October 13

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumanne October 13, 2020

1. Manchester United imeweka mipango ya kumsainisha kiungo wa Rennes na Ufaransa Eduardo Camavinga, 17, iwapo mfaransa mwenzie Paul Pogba, 27, ataamua kuondoka Old Trafford, Manchester United huenda ikakabilana na Real Madrid katika kumuwania Camavinga.

2. Mshambuliaji wa zamani wa Manchester City na Brazil Robinho, 36, amejitolea kupokea mshahara wa £200 tu kwa mwezi akirejea kwa awamu ya nne kwenye klabu yake ya utotoni Santos.

3. Uhamisho wa mshambuliaji wa Algeria Said Benrahma wa £25m kutoka Brentford kwenda West Ham uko hatarini kuvunjika, ambapo wapiga nyundo hao wamejielekeza zaidi kwa mshambuliaji wa Bournemouth raia wa Norway Josh King, 28.

4. Crystal Palace huenda ikapeleka ofa ya lala salama kumnasa Benrahma, 25. Fulham wako katika hatua nzuri ya mazungumzo ya kumsajili mlinzi wa Huddersfield na Uholanzi Terence Kongolo, 26. 

5. Wachezaji kadhaa wa Manchester United wameeleza masikitiko yao ya namna hali inavyomwendea mlinda mlango wa timu hiyo muargentina Sergio Romero, 33, ambaye amekosa nafasi Old Trafford baada ya kurejea kwa Dean Henderson, lakini uhamisho wake wa siku ya mwisho kushindikana kufuatia ada iliyowekwa ya £10m.


EmoticonEmoticon