Tetesi Za Soka Ulaya Ijumaa October 9, 2020
1. Mshambuliaji wa Wales Gareth
Bale, 31, anataka kushinda taji la Uingereza msimu huu akiichezea Tottenham,
kulingana na ajenti wake.
2. Arsenal inataka kuanzisha
mazungumzo na Mesut Ozil kuhusu kufutilia mbali kandarasi yake kabla ya dirisha
la uhamisho la mwezi Januari.
3. Manchester United itajaribu
kumsaini beki wa RB Leipzig na Ufaransa Dayot Upamecano, 21, kwa dau la £36.5m
msimu ujao.
4. Liverpool na Manchester City
zina hamu ya kumsajili. Liverpool itafanya mazungumzo na winga Harry
Wilson kuhusu uwezekano wa uhamisho wa mkopo katika klabu nyengine muda tu
mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 atarudi baada ya mechi ya kimataifa
akiichezea.
5. West Ham inafikiria usajili wa £5m wa kiungo wa kati wa QPR na Ireland Ryan Manning. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 pia anaweza kucheza kama beki wa kushoto.
EmoticonEmoticon