Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Ijumaa October 16

 

Tetesi Za Soka Ulaya Ijumaa October 16, 2020

1. Juventus wanapanga uhamisho wa £360m kumnasa mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, 21, klabu hiyo ya Serie A inaweza kumpeleka Cristiano Ronaldo upande wa pili.

2. Klabu ya Ujerumani ya Borussia Dortmund haina mpango wa kumuuza winga wa England Jadon Sancho, 21, katika dirisha dogo la usajili la January, ambaye alihusishwa na Manchester United katika majira ya joto. 

3. Na Chelsea walikuwa tayari kumlipa mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi, 33, mshahara wa £1m kwa wiki kwa uhamisho wenye thamani ya £225m mwaka 2014.

4. Arsenal inataka kuipiku Manchester United katika kumsajili mlinzi wa Villarreal, Pau Torres, 23, kwa kitita cha £35m mwezi January. 

5. Kuingo wa Manchester United Bruno Fernandes, 26, amekataa kumnyooshea kidole Ole Gunnar Solskjaer na wachezaji wenzake baada ya kipigo cha 6-1 kutoka kwa Tottenham kabla ya mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa.


EmoticonEmoticon