Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumanne October 06

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumanne October 6, 2020

1. Maafisa wakuu wa klabu ya Manchester United wamewasiliana na aliyekuwa kocha wa Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino iwapo watamfuta meneja Ole Gunnar Solskjaer. 

2. Manchester City imekataa ofa ya dau la £15.4m na marupurupu kutoka kwa klabu ya Barcelona kumnunua beki wa Uhispania Eric Garcia, 19, katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho.

3. Liverpool ilipokea maombi ya winga wa Switzerland Xherdan Shaqiri, 28, wakati wa dirisha la uhamisho na wanataraji atasalia katika klabu hiyo hadi mwezi Januari kwasasabu hawako tayari kumuuza kwa mkopo .

4. Barcelona imepoteza zaidi ya £181m kama mapato kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

5. Mkufunzi wa Paris St-Germain Thomas Tuchel hafurahii hatua ya klabu hiyo kushindwa kununua wachezaji katika dirisha la uhamisho. 


EmoticonEmoticon