Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Alhamisi October 1

 

Tetesi Za Soka Ulaya Alhamisi October 1, 2020

1. Manchester United imeanza mazungumzo na Barcelona kuhusu kumnyakua kwa mkopo mshambuliaji Mfaransa Ousmane Dembele 23.

2. Liverpool wanajiandaa kukubali ofa ya pauni milioni 23 kutoka Sheffield kwa ajili ya mshambuliaji Rhian Brewster. 

3. Chelsea inaweza kuongeza wachezaji wa kuondoka kwenye klabu hiyo kwa kumuuza mlinzi Mhispania Marcos Alsonso, 29, beki wa kati Antonio Rudiger, 27, na kiungo wa kati Ruben Loftus-Cheek, 24 kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili. 

4. Tottenham wamemaliza makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Benfica Carlos Vinicius,25, kwa mkopo, ambaye gharama ya kuondoka kwake ni kiasi cha pauni milioni 89 kwa mujibu wa kufungu cha mkataba wake.

5. Arsenal wako kwenye mazungumzo ya kumtoa kwa mkopo kiungo wao wa kati Matteo Guendouzi kwenda Marseille.


EmoticonEmoticon