Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumamosi October 10

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumamosi October 10, 2020

1. Manchester City itaweza kumsajili kiungo mchezeshaji kutoka Barcelona, Muargentina Lionel Messi, 33, msimu ujao kama fursa hiyo itajitokeza, anasema Afisa mkuu uendeshaji Omar Berrada.

2. Mshambuliaji wa Borussia Dortmund, raia wa Norway striker Erling Haaland, 20, na winga wa klabu hiyo, kutoka England Jadon Sancho, 20, bado wako kwenye orodha kuu ya Ole Gunnar Solskjaer ndani ya Manchester United.

3. Real Madrid imeoondoa uwezekano wa kumsajili kiungo wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 27, baada ya kusema ilikuwa ndoto yake kuchezea klabu hiyo siku moja. 

4. Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 31, anajiandaa kucheza mchezo wake wa kwanza wakati huu akirejea kuichezea Tottenham kwa mara ya pili dhidi ya West Ham mwishoni mwa wiki ijayo. 

5. Manchester City wana matumaini Pep Guardiola atasaini mkataba mpya, lakini watatafuta mrithi wake iwapo meneja huyo ataonyesha dalili za kutaka kuondoka.


EmoticonEmoticon