Tetesi Za Soka Ulaya Jumatatu October 12, 2020
1. Mkufunzi wa Inter Milan Antonio
Conte ana mpango wa kuwasilisha ombi la kumsajili mshambuliaji wa Manchester
City na Argentina Sergio Aguero, 32, ambaye kandarasi yake inatarajiwa
kukamilika mwisho wa msimu huu.
2. Manchester City iliamua kumzuia
beki wa Uhispania Eric Garcia kwa msimu mmoja kwasababu alikuwa na thamani
kubwa kwao zaidi ya ofa ya Barcelona ya £18m , kulingana na ofisa wa operesheni
Omar Berrada.
3. Garcia, 19, anaweza kuhamia Nou
Camp kwa uhamisho wa bila malipo msimu ujao baada ya kukataa kandarasi.
4. Mkufunzi wa Barcelona Ronald
Koeman anasema kwamba mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez, 33, angesalia katika
uwanja huo ili ili kuthibitisha umuhimu wake badala ya kuhamia Atletico Madrid.
5. West Ham wanakaribia kukubaliana dau la uhamisho la £25m kumsajili Benrahma kwa kutoa pamoja na marupurupu.
EmoticonEmoticon