Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumatano October 14

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumatano October 14, 2020

1. Barcelona wanaandaa kuwanasa nyota wawili Pogba na kiungo wa Bayern Munich na Austria David Alaba, 28.

2. West Ham na Brentford zimekubaliana kuhusu uhamisho wa £30m wa mshambuliaji Said Benrahma, 25, lakini bado kukubaliana maslahi binafsi na mshambuliaji huyo wa Algeria.

3. Mlinda mlango wa Manchester United Muargentina Sergio Romero, 33, anataka kuvunja mkataba mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi huu, akitaka kuhamia ligi ya Marekani.

4. Crystal Palace wanakaribia kukamilisha uhamisho wa mkataba mfupi wa beki wa kulia Nathaniel Clyne, 29, ambaye ni mchezaji huru kwa sasa baada ya kuondoka Liverpool kwenye majira ya joto.

5. Leeds United wanamuania kiungo wa Norwich City na timu ya England chini ya miaka 21, Todd Cantwell, 22, pamoja na kiungo wa Derby County na England chini ya miaka 19 Louie Sibley, 19.


EmoticonEmoticon