Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Alhamisi October 3

 

Tetesi Za Soka Ulaya Alhamisi October 15, 2020

1. Kiungo wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 27, anataka kujiunga na Barcelona kwa uhamisho huru dirisha lilajo la usajili la majira ya joto.

2. Kiungo wa Arsenal, mjerumani Mesut Ozil, 31, mapema mwezi huu alikataa ofa ya mshahara wa £200,000 kwa wiki kuondoka kwa washika bunduki hao na kutua ligi ya Saudi Arabia.

3. Meneja wa zamani wa Juventus Max Allegri anaweza kuwania nafasi ya Ole Gunnar Solskjaer , kama Manchester United itamtimua kocha wake huyo. 

4. Juventus imeungana na Manchester City katika mbio za kumuania mlinzi wa Bayern Munich na Austria David Alaba, 28. 

5. Chelsea wanajiandaa kuanza mazungumzo ya kuongeza mkataba na kiungo wake kutoka Italia, Jorginho, ambaye alihusishwa na mipango ya kuhamia Arsenal wakati wa dirisha la usajili lililopita.


EmoticonEmoticon