Tetesi Za Soka Ulaya Jumatatu October 19, 2020
1. Manchester United imepewa
tumaini kwamba inaweza kusaini mkataba na winga wa Borussia Dortmund na England
Jadon Sancho, 20, baada ya 'kumuhukumu vibaya' alipomtaka msimu uliopita.
2. Man United pia wanamlenga
kiungo wa kati wa Sporting Lisbon mwenye umri wa miaka 16-Luis Gomes. Kiungo
huyo wa safu ya kati Mreno amepewa jina la ' Luis Figo' ajaye nchini mwake.
3. Winga wa Wolves Adama Traore,
24, yuko tayari kupokea wito Barcelona na Liverpool ili kusaini mkataba mpya wa
pauni 100,000-kwa wiki katika Molineux.
4. Mchezaji na kocha wa Derby
County Wayne Rooney, mwenye umri wa miaka 34, anatarajia kupata matokeo ya
vipimo vya Covid-19 test Jumatatu baada ya kugundua kuwa rafiki yake
aliyemuuzia saa ya mkononi alikuwa na virusi vya corona.
EmoticonEmoticon