Tetesi Za Soka Ulaya Jumatano October 21, 2020
1. Mlinzi wa zamani wa Arsenal Per
Mertesacker anasema kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil mawazo yake yapo
mbali mpira wa miguu - mchezaji huyo wa miaka 32 ameachwa kwenye kikosi cha
Washika Bunduki cha Ligi Kuu ya siku ya Jumanne.
2. Tottenham wapo mbioni kuingia
mkataba mpya wa muda mrefu na mshambuliaji wa Korea Kusini Son Heung-min, 28.
3. Manchester City wako wazi
kumpokea Pablo Zabaleta anayerejea katika klabu hiyo kuchukua wadhifa ambao sio
wa kimchezo kufuatia kustaafu kwa Muagentina huyo mwenye umri wa miaka 35-wiki
iliyopita.
4. Beki wa zamani wa Manchester
United, Rio Ferdinand anaamini meneja Ole Gunnar Solskjaer amesikitishwa na
jinsi bodi ya timu hiyo ilivyoshindwa kufikia malengo yao juu ya uhamisho
kwenye dirisha la msimu wa joto.
5. Kocha wa Union Berlin Urs Fischer amekiri kwamba mlindalango wa Liverpool anayecheza kwa deni Loris Karius hakufurahi kwa kuachwa kwa benchi dhidi ya Schalke na anatumaini kuwa Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 27-ataonesha mchezo wake.
EmoticonEmoticon