Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumatatu October 26

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumatatu October 26, 2020

1. Mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala 26 ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Tottenham pamoja na Man United yuko katika mazungumzo ya kuandikisha mkataba mpya na klabu hiyo ya Itali.

2. Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 21,ana mipango ya kushinda kombe la mabingwa Ulaya akiwa na klabu ya PSG kabla ya kuhamia katika klabu nyengine kubwa, kulingana na kiungo wa kati aliyeichezea PSG na ambaye sasa ni balozi wa klabu hiyo Youri Djorkaeff.

3. Manchester United ilikosa kumsajili beki wa RB Leipzig na Ufaransa mwenye umri wa miaka 21 Dayot Upamecano - ambaye kwa sasa ana thamani ya £55m - kwasababu ya mgogoro kuhusu £200,000 miaka mitano iliopita .

4. Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta anasema kwamba amekuwa wazi na kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil, 32, licha ya ajenti wa mchezaji huyo kudai kwamba kumekuwa hakuna uwazi kuhusu mchezaji huyo kuwachwa nje ya kikosi cha timu hiyo.

5. Mshambuliaji wa Poland Arkadiusz Milik, ambaye alikuwa tayari kujiunga na Juventus msimu ujao ataondoka Napoli mwezi Januari huku klabu za Tottenham na Everton zikimnyemelea mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.


EmoticonEmoticon