Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumatano October 7

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumatano October 7, 2020

1. Manchester United imejiondoa katika kumsaini mshambuliaji wa England Jadon Sancho 20, baada ya kubaini kwamba uhamisho huo huenda ukaigharimu timu hiyo £227m kutokana na dau la £108m linalotakiwa na Borussia Dortmund , pamoja na mahitaji ya marupurupu ya mshahara kutoka kwa ajenti wake.

2. West Ham walikuwa wako tayari kumsaini beki wa England Fikayo Tomori, 22, kwa mkopo ambao walikuwa wamejitolea kuilipa Chelsea dau la £50,000 kila mara alipokosa kuwachezea The Hammers , lakini makubaliano hayo hayakuafikiwa.

3. Tottenham na West Ham wana hamu ya beki wa kati wa Wales Joe Rodon, 22, na huenda wakawasilisha ombi la dau la £18m kabla ya siku ya mwisho ya ligi ya EFL mnamo tarehe 16. 

4. Ombi la Manchester United la kumsajili winga wa Senegal Ismaila Sarr kwa kipindi kilichosalia cha msimu huu lilikataliwa na Watford , lakini inaweza kujaribu tena mwezi huu licha ya kwamba The hornets wanataka mkataba wa kudumu.

5. Barcelona itasubiri hadi mwisho wa msimu wa 2021 ili kumsajili beki wa Uhispania Eric Garcia, 19, kutoka Manchester City. Barca ilitoa Yuro milioni 2 katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho.


EmoticonEmoticon